WILAYA
YA MOMBA - UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA .
MNAMO TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA
19:45HRS HUKO KATIKA ENEO LA SOGEA –
MAKAMBINI, KATA YA TUNDUMA,
TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA, ALPHONCE S/O MWANJELA, MIAKA 36, KYUSA, MFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA, MKAZI WA SOGEA –
MAKAMBINI ALIVAMIWA NA KUNDI LA WATU
WANNE WASIOFAHAMIKA KISHA KUMKATA MAPANGA KICHWANI NA KUMJERUHI KWA KUMPIGA
RISASI MGUU WA KULIA KWA KUTUMIA BUNDUKI IDHANIWAYO KUWA S/GUN NA KUMPORA PESA TASLIMU TSHS
5,200,000/=, USD 2,300, RAND 10,000 NA ZAMBIA KWACHA 2,000,000. WATUHUMIWA HAO
WALIMVAMIA MHANGA AKIWA UMBALI WA MITA
50 TOKA NYUMBANI KWAKE WAKATI ANATOKA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KUBADILISHA
FEDHA MPAKANI TUNDUMA. MHANGA AMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA HALI YAKE
INAENDELEA VIZURI. MSAKO MKALI UNAENDELEA DHIDI YA WAHUSIKA WA TUKIO HILI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA WAJIUNGE PAMOJA
WAFUNGUE DUKA LA KUBADILISHA FEDHA AMBALO LITAKUWA LIMESAJILIWA ILI ULINZI UWE
RAHISI ILI KUONDOA SUALA LA KUTEMBEA NA FEDHA KIHOLELA NA KUFANYA WIZI/UPORAJI
NA UNYANG’ANYI KUWA RAHISI. PIA ANATOA WITO KWA WALE WANATAKA KUBADILISHA FEDHA WAENDE KATIKA TAASISI RASMI ZA
KUBADILISHA FEDHA KWA USALAMA ZAIDI KWANI UWEZEKANO WA KATAPELIWA NI MDOGO. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA
YA CHUNYA – TAARIFA YA KIFO.
MNAMO TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA
16:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA CHOKAA, KIJIJI CHA KIBAONI, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, EZEKIA D/O AZIGETI, MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI CHOKAA, ALIKUFA
MAJI WAKATI AKIOGELEA NA WATOTO WENZAKE KWENYE MTO CHUNYA. CHANZO NI BAADA YA
MAREHEMU KUZIDIWA NA MAJI WAKATI AKIOGELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI
KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA
KUTOWARUHUSU KWENDA KUOGA KATIKA MITO/MABWAWA/MATIBWI YA MAJI. AIDHA ANATOA
WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA NA KUZIBA MASHIMO NA VISIMA VILIVYOWAZI ILI
KUEPUKA MATUKIO YA WATOTO WADOGO KUFA MAJI.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE].
MNAMO TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA
12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA MANDA “B”, KIJIJI NA KATA YA GUA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA KWA USHIRIKIANO NA WAHIFADHI WA HIFADHI
YA NGWALA WALIMKAMATA OCTAVIAN S/O
ISMAIL, MIAKA 38, MBUNGU AKIWA NA SILAHA
GOBOLE MOJA KINYUME NA SHERIA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA
ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
[BARAKAEL
MASAKI – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon