TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06. 12. 2013.



WILAYA YA MBARALI – AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                          NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 05.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTAMBALA, KATA YA MAPOGORO, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA, PIKIPIKI T.353 CMN AINA YA  SUNLG IKIENDESHWA NA MUDA S/O MAPANDE, MIAKA 28, MBENA, MKAZI WA UTULO ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO RAHABU D/O HAMISI, MIAKA 4, MBENA, MKAZI WA MTAMBALA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI HASA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2013 KWANI AJALI ZINAUA NA KUSABABISHA MADHARA KWA FAMILIA NA TAIFA KWA UJUMLA. AIDHA ANATOA WITO KWA ABIRIA WA PIKIPIKI KUVAA HELMENT NA KUTOSHABIKIA MWENDO KASI KWANI UNAUA. PIA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA NA UANGALIZI WA WATOTO WADOGO HASA KIPINDI HIKI CHA MWISHO WA MWAKA.

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA POWERTILLER KUGONGANA NA PIKIPIKI NA 
                                          KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 05.12.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA UBARUKU, KATA YA RUJEWA, TARAFA YA  RUJEWA, WILAYA YA  MBARALI, MKOA WA MBEYA, PIKIPIKI T.745 BAD AINA YA  SAN-MOTO  IKIENDESHWA NA WILSON S/O MGENI, MIAKA 36, MKINGA, MKAZI WA UTYEGO ILIGONGANA NA POWERTILLER AINA YA  KUBOTA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SHADRACK S/O NZILUKA, MIAKA 25, MBENA, MKAZI WA MAJENGO  NA KUSABABISHA KIFO CHA AMON S/O MGUTE, MIAKA 22, MBENA, MKAZI WA MAJENGO AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKI HIYO.  CHANZO KINACHUNGUZWA. SHADRACK S/O NZILUKA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MTUHUMIWA MMOJA AMEKAMATWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI HASA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2013 KWANI AJALI ZINAUA NA KUSABABISHA MADHARA KWA FAMILIA NA TAIFA KWA UJUMLA. PIA ANATOA WITO KWA ABIRIA NA WAENDESHA PIKIPIKI KUVAA HELMENT NA KUTOSHABIKIA MWENDO KASI KWANI UNAUA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA MWINGINE WA AJALI HII AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.



[BARAKAEL MASAKI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »