WILAYA YA CHUNYA –
MAUAJI.
MNAMO TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA
08:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ITEGE,
KIJIJI CHA ITINDI, KATA YA GALULA, TARAFA YA SONGWE,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, NYESI
D/O MPONJA, MIAKA 25, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI ALIFARIKI
DUNIA WAKATI ANAPELEKWA KITUO CHA AFYA MBUYUNI KWA MATIBABU BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NGUMI, MATEKE NA
UBAO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE NDELE S/O JULIUS, MIAKA 43, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
ITINDI. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA
WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA
MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
WILAYA
YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA
08:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA
TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA
WA MBEYA, EDDY S/O MBILINYI, MIAKA 34, MKINGA, MFANYABIASHARA YA NGUO ZA MITUMBA, MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI
DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA
KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE TAREHE 14.12.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS KATIKA KIJIJI CHA MBEYE-ONE, KATA YA ISONGOLE,
TARAFA YA UKUKWE, KWA TUHUMA ZA
KUVUNJA DUKA USIKU NA KUIBA NGUO ZA AINA MBALIMBALI MALI YA ZIDI
S/O JULIUS. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO WAKAMATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WILAYA
YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA
KIFO
NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA
11:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA NEWLAND,
KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA,
GARI T.668 CGY/T.702 CGZ AINA
YA FAW
MALI YA KAMPUNI YA SILENT ROAD HAULAGE LIKIWA LIMEPAKIA
MBOLEA TOKA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI
LIKIENDESHWA NA DEREVA KUDRA S/O
RAMADHAN, MIAKA 35, MLUGURU, MKAZI WA UBUNGO- DSM LILIACHA NJIA NA
KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA TINGO WA GARI HILO MATHIAS S/O JOEL MWENDA, MIAKA 31, MLUGURU, MKAZI WA CHAMAZI –DSM
PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA DEREVA WA GARI HILO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI
YA MISHENI
IGOGWE. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL MASAKI– ACP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon