TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 04.12. 2013.


         



WILAYA YA  MBARALI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE  02.12.2013 MAJIRA YA  SAA 07:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIJIJI CHA LEMBUKA- IYAMBOGO, KATA YA  CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIWAKAMATA 1. BERETE S/O TEFRA, MIAKA 24, 2. SAMWEL S/O GIRMA, MIAKA 30 NA 3. MUATU S/O BALAGALA, MIAKA 23 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA  KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO IKIWA NI PAMOJA NA KUKAMATWA.



[BARAKAEL MASAKI   - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »