Serikali
yaandaa siku 11 za kuruhusu dunia kuuaga mwili wake
Afrika
na dunia inatarajiwa kushuhudia kitu kipya katika maziko ya Rais wa zamani wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela (95) aliyefariki dunia juzi, baada ya kuugua kwa
zaidi ya miezi sita.
Serikali
ya Afrika Kusini imesema kiongozi huyo ambaye atazikwa Desemba 15, imeandaa
mazishi ya kihistoria yanayosemekana yatazidi yale ya Papa John 11.
Matukio
ya shughuli mbalimbali zinazohusu mipango ya maziko ya kiongozi huyo maarufu
yanatarajiwa kushuhudiwa sehemu mbalimbali duniani, tofauti na tukio jingine
lililowahi kutokea barani Afrika mbali na kombe la dunia.
Rais
Jacob Zuma alisema jana kwamba “Mpendwa wetu Madiba atazikwa kwa heshima zote
za Serikali. Nimeagiza bendera zote za Afrika Kusini zipepee nusu mlingoti na
hiyo itaendelea hivyo hadi tutakapokamilisha mazishi yake.
Mazishi
ya Mandela yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo
yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais
wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili.
Yanakadiriwa pia kulingana na maziko ya Winston Churchil aliyekuwa Waziri Mkuu
wa Uingereza mwaka 1965.
Marais
wote wa Marekani walio hai wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo iwapo afya zao
zitawaruhusu kusafiri, pamoja na Prince Charles wa Uingereza na hata Rais Robert
Mugabe wa Zimbabwe. Pia watu maarufu wenye urafiki wa karibu na Mandela akiwamo
msanii Oprah Winfrey wameshathibitisha kuhudhuria.
Changamoto
la kiusalama
Kutokana
na idadi kubwa ya wakuu wa nchi na watu maarufu duniani wanaotarajiwa kufika
Afrika Kusini, suala la usalama limeelezewa kuwa changamoto mpya kwa vyombo vya
usalama nchini humo.
Afrika
Kusini imekuwa moja ya nchi zinazokabiliwa na matukio ya uporaji na mauaji
yanayotokana na idadi kubwa ya wahalifu, wengi wao wakidaiwa kuwa wahamiaji
haramu.
“Huyu
ni shujaa wa dunia. Tutafanya mipango ya mazishi makubwa ambayo hayajawahi
kushuhudiwa. Nadhani kila nchi itakuwa imeandaa utaratibu wake wa namna ya
kushiriki,” alisema mmoja wa wanadiplomasia wa Afrika Kusini ambaye hakutaka
kutajwa jina lake.
Siku
11 za maombolezo
Serikali
ya Afrika Kusini, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian tayari imeweka wazi
ratiba ya siku 11 za maombolezo tangu alipofariki dunia juzi jioni. Japokuwa
ratiba hiyo ilishaandaliwa karibu mwaka mmoja uliopita na kupitiwa na kufanyiwa
maboresho katika baadhi ya maeneo, inaonyesha namna maofisa wa Serikali ya
Afrika Kusini walivyolipa uzito suala hilo na kulifanya kuwa tukio la
kukumbukwa katika historia.
“Mwili
wake ulipelekwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti kwa ulinzi wa polisi jana, na
tayari mipango yote ya kurusha moja kwa moja kupitia shughuli hii kupitia
televisheni imekamilika,” inasomeka taarifa ya Serikali.
Taarifa
ya Serikali iliyotolewa jana pia ilieleza kwamba tayari vitabu kwa ajili ya
rambirambi vimeshaandaliwa katika ofisi zote za ubalozi, kwenye ofisi za Nelson
Mandela Foundation, majengo yote ya Serikali na kwenye sehemu ya kumbukumbu ya
Mandela huko Soweto.
Katika
siku ya tatu, yaani leo wanadiplomasia wa nchi mbalimbali waliopo nchini
humo
watapewa
taarifa mjini Pretoria kuhusu utaratibu wa mazishi ya Mandela na katika siku ya
nne, yaani kesho watu mbalimbali mashuhuri wataruhusiwa kuitembelea familia ya
Mandela.
Katika
siku ya tano na ya sita kutakuwa na sala maalumu ya kumbukumbu ya Mandela
itakayohudhuriwa na watu mbalimbali na viongozi wa makundi yote ya kijamii
ambapo mwili wa kiongozi huyo mwenye historia ya kipekee duniani pia utawekwa
mbele ya hadhira.
Tukio
hilo litahudhuriwa pia na Rais Jacob Zuma na zitawekwa ‘skrini’ za televisheni
katika baadhi ya kumbi za manispaa na viwanja vya wazi huko Soweto, Cape Town
na maeneo mengine kwa ajili ya kuwezesha watu wengi kushuhudia shughuli zote za
mazishi.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo, siku ya nane mwili wa Mandela utawekwa kwenye jengo la
Serikali mjini Pretoria kwa siku tatu mfululizo, ili kutoa fursa kwa wananchi
kuuaga.
“Mwili
huo utawekwa katika eneo hilo kuanzia asubuhi hadi jioni kwa siku zote tatu
ukiwa ndani ya jeneza la kioo ili kuruhusu watu kuuona, kisha utaondolewa kwa
ajili ya kuandaliwa kwa siku inayofuata…
Katika
siku ya tisa, Jeshi la Afrika Kusini litaendelea kusimamia na kutoa heshima za
mwisho na kufanya maandalizi ya mazishi rasmi ya kitaifa kwenye jengo la Union
Buildings ambapo Mandela aliapishwa rasmi kuwa rais wa kwanza mweusi
aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1994.
Pia
shughuli ya kuwapokea wakuu wa nchi mbalimbali watakaoshiriki katika maziko
hayo itakuwa ikiendelea.
Katika
siku ya 10 baadhi ya mitaa itafungwa ikiwa ni hatua ya kuimarisha zaidi ulinzi
na maandalizi ya mwisho ya eneo la kuuaga mwili huo kwenye Union Building,
ambapo jeshi litakuwa likikamilisha kuandaa vifaa vyote vitakavyotumika wakati
wa maziko yake, kisha mwili wake utachukuliwa na kwenda kuandaliwa rasmi kwa
ajili ya kuhitimisha maziko.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, mwili huo utawekwa rasmi kwenye eneo hilo siku ya 11 na
kuwaruhusu wakuu wa nchi na wageni mbalimbali wa kimataifa watakaokuwa wamefika
kumuaga hayati Madiba na baadaye kuhudhuria mazishi hayo.
Taarifa
hiyo imeeleza kwamba baada ya kutoa fursa kwa wakuu wa nchi kutoa heshima zao
za mwisho safari ya kuelekea kijijini Qunu ambako ndiko alikozaliwa itaanza
siku ya 11 kwa ajili ya kuupumzisha kwa amani, kazi ambayo itasimamiwa na
jeshi.
Taarifa
hiyo inaeleza kwamba katika siku ya mwisho, asubuhi mwili huo utapitishwa katika
baadhi ya mitaa kwenye Kijiji cha Qunu kisha kupelekwa katika eneo la nyumbani
kwa Mandela na siyo katika makaburi ya familia ya Mandela.
Wageni
wanaotarajiwa kuhudhuria mazishi ya Mandela ni pamoja na Rais Barack Obama wa
Marekani na mkewe Michelle ambaye aliwahi kumtembelea Mandela nchini Afrika
Kusini mwaka 2011 pamoja na binti zake, Sasha na Malia.
Pia
rais wa zamani, Bill Clinton na mkewe Hillary ambao wamekuwa marafiki wa karibu
wa Mandela wanatajwa kuwa miongoni mwa watakaohudhuria maziko yake, pamoja na
marais wengine wastaafu wa Marekani.
Chanzo
kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Afrika Kusini kilisema Prince Charles na
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wamethibitisha kwamba watahudhuria.
Mgogoro
wa familia
Moja
ya mambo yanayotarajiwa kuibua utata katika mpango huo wa karibu wiki mbili za
maandalizi ya mazishi ni mvutano katika familia ya marehemu Mandela.
Mjukuu
wake ambaye ndiye kiongozi wa familia, Mandla amekuwa akituhumiwa kufanya
mkakati wa kumzika Mandela kwenye Kijiji cha Mvezo ambako anatambulika kama
chifu wa eneo hilo.
Wanafamilia
wengine pamoja na serikali ya nchi hiyo wamekuwa wakidai kwamba eneo
linalostahili kuzikwa Mandela ni Kijiji cha Qunu ambako amekuwa akiishi tangu
alipostaafu.
EmoticonEmoticon