HIZI AJALI NI NINI JAMANIIIIIIIIIIIIIIIIIII KWANINI MADEREVA HAWAJIFUNZI

 LORI LILILOBEBA BIA LAPINDUKA MADABA SONGEA.

 
Ajali ya lori lililobeba bia imetokea leo Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea tarafa ya Madaba kata ya Mkongotema, mdau wetu aliyepita eneo hilo amezidaka picha hizi za tukio na haijafahamika mara moja kama ajali hiyo imesababisha vifo ama majeruhi.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


2.Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Simiyu express lililokuwa likitokea mkoani Simiyu kuelekea jijini Dar es salaam baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Ihumwa manispaa ya Dodoma.



3.


Watu 12 wamekufa na wengine 44 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Burdan linalofanya safari zake kutoka wilayani Korogwe kwenda jijini Dar es salam kuacha njia kisha kupinduka.
Ajali hiyo imetokea eneo la kijiji cha Taula kilichopo kata ya Kwedizinga wilayani Handeni katika barabara kuu inayounganisha Chalinze-Segera ambapo inadaiwa kuwa dereva wa basi hilo ambaye ni miongoni mwa marehemu alikwaruzwa na lori wakati alipokuwa akilipita lori kubwa aina ya Fuso ndipo gari lilipomshinda na kusababisha kwenda katika bonde lililopo pembeni mwa barabara hiyo.
Baadhi ya watu waliokua majeruhi katika eneno la tukio wamesema waliokufa pale pale baada ya gari kupinduka walikuwa sita lakini wengine waanne walikuwa katika hali mbaya ndipo wakati wakiwa katika harakati za kuwawahisha hospitali walipoteza maisha.
Kwa upande wa daktari wa zamu aliyepokea miili ya marehemu na majeruhi katika hospitali teule ya wilaya ya Korogwe ya Magunga Dr, John Hedes hakusita kuwataja waliofariki dunia kwa majina ambapo ni wanaume sita na wanawake sita huku wengine sita wamejeruhiwa vibaya na kuhamishiwa katika hospitali za rufaa za KCMC na Muhimbili.
Kufuatia hatua hiyo,kamanda wa polisi mkoani Tanga Costantine Massawe amewataka abiria wanaosafiri katika mabasi ya kampuni mbali mbali mkoani Tanga kupiga namba za simu za askari yeyote alieyeko katika eneno lao ili dereva anayekwenda mwendo kasi aweze kukamatwa.
Tayari rais Jakaya Kikwete amemtumia mkuu wa mkoa wa Tanga salam za rambirambi kufuatia ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 12 na kujeruhi wengine 44.
Previous
Next Post »