Facebook yazindua alama ya 'Dislike' kama mbadala wa 'Like', kuanza kutumika kupitia Facebook Messenger


Hatimaye watumiaji wa mtandao wa Facebook wamepata mbadala wa alama ya ‘Like’ baada ya wamiliki wa mtandao huo wa kijamii kuzindua alama ya ‘Dislike’, lakini kwa kuanza alama hiyo inatumika kupitia huduma ya ‘Facebook Messenger’.
Mtandao huo umeweka alama ya dole gumba likiwa linaangalia chini kuonesha kuwa mtumiaji hakupenda ile post, ikiwa ni mbadala wa alama ya kupenda ‘Like’.
Mtandao huo pia umezindua sticker nyingine kama alama ya amani, alama ya ngumi kuonesha kuwa unapingana na swala hilo (protest), alama ya mkono uliobeba maua, na glass ya Champagne.
Previous
Next Post »