
Ajali hiyo imesababisha dereva kupoteza maisha na kuacha vipande vya ubongo vikining’inia katika moja ya madaraja hayo, baada ya gari hilo aina ya Toyota Celica GTR lenye namba za usajili T220ABL kugonga na kisha kuingia kwenye ukingo wa daraja na kisha kutumbukia kwenye mto. Maiti iliondolewa asubuhi wakati ajali hiyo ilitokea kati ya saa 8 na saa 9 alfajiri.




Ajali mbaya na ya kutisha imetokea leo alfajiri katikati ya madaraja mawili ya chuma yaliyoko eneo la Kawe pembeni ya kambi ya JKT Mlalakuwa, Dar es Salaam.
Ajali hiyo mbaya iliyotokea na kusababisha dereva kupoteza maisha na kuacha vipande vya ubongo vikinin'ginia(PICHA YA 9) katika moja ya madaraja hayo, ilitokea wakati derevea huyo akiwa kwenye mwendo mkali na kushindwa kulimudu gari hilo aina ya Toyota Celica GTR yenye namba za usajili T220ABL(PICHA YA 11) na kuingia kwenye ukingo wa daraja(PICHA 2) na kisha kutumbukia kwenye mto unaopeleka maji baharini.
Inadaiwa maiti iliondolewa asubuhi wakati ajali hiyo ilitokea kati ya saa 8 na saa 9 alfajiri.





Mmoja wa mashuhuda (alikataa kutaja jina lake) akitoa vipande vya nguo katika sehemu ya nyuma ya gari hilo kama alivyokutwa na mpiga picha wetu
Juu na Chini: Picha inayoonesha kipande cha nyama inayodaiwa kuwa ni sehemu ya ubongo wa dereva huyo kikiwa kinanin'ginia katika daraja hilo. chini ni sehemu ya kioo cha mbele kilicho haribiwa vibaya na kubaki na sehemu ya damu
Habari kwa mujibu wa Imma Matukio blog (bofya hapa kuona picha zaidi).
x









Habari kwa mujibu wa Imma Matukio blog (bofya hapa kuona picha zaidi).
EmoticonEmoticon