WASAKWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI MBEYA





Na Saimeni Mgalula,Mbeya

Jeshi la polisi Mkoani hapa linawatafuta Mama na Mtoto wake kwa tuhuma
za mauaji ya Silevesta Alfonsi (55) mkazi wa Ichesya Wilayani chunya
mkoani hapa ambaye ni mume wa mtuhumiwa.

Akizungumzia kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa huu
kamishina Msaidizi wa polisi Diwani Athumani alisema Kurusina Korineli
(42) na Mwanae Kondo Silivesta (19) walimshambulia marehemu kwa
kumpiga Rungu kichwani na na Utosini pamoja na ngumi na kumsababishia
kifo chake papo hapo na watuhumiwa walikimbia walipi baini ameuawa .

Kamanda Athumani alisema inasadikika kuwa chanzo cha mauaji hayo ni
wivu wa kimapenzi kufuatiwa na marehemu kuongea na mwanamke mwingine
wakati wakiwa kilabuni na mbinun waliotumia ni kumshambulia kwa
kumpiga baada ya kufika nje ya nyumba wakitoka kwenye kilabu cha pombe
za kienyeji.

Tukio hilo lilitokea Novemba 12 mwaka huu saa 2:oo asubuhi kijijini
hapo na Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa
walio tenda tukio hilo ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola
kujibu mashtaka yanayo wakabili.

Previous
Next Post »