WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA
18:30HRS HUKO MBALIZI KATA YA BONDE
LA USONGWE, TARAFA YA USONGWE BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, GARI T.318 BHS/T.897 BMG AINA YA
BENBEN LIKIENDESHWA NA DEREVA
NURDIN S/O YUSUPH, MIAKA 33, MNGONI, MKAZI WA DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU ELIZA D/O LOFA, MIAKA 60,
KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA IFISI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA
15:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA KILIMANJARO –TUNDUMA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, GARI
T.211 ACB AINA YA VOLVO LIKIENDESHWA
NA DEREVA GWELOMO S/O KALINGA, MIAKA
34, MHEHE, MKAZI WA DSM LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI
YA MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA AMEKAMATWA NA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MSUKUMA MKOKOTENI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA
19:30HRS HUKO IGURUSI KATA YA IGURUSI,
TARAFA YA ILONGO BARABARA YA MBEYA/NJOMBE
WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA, GARI
T.284 BNZ/T.638 BPF AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA
NA DEREVA MBITA S/O SAID, MIAKA 35,
MYAO, MKAZI WA MBEYA, LILIMGONGA MSUKUMA MKOKOTENI KIBOSI S/O MWAIPUNGU, MIAKA 35, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA
IGURUSI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI
ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
MISHENI CHIMALA. CHANZO MWENDO
KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[BARAKAEL
MASAKI – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon