TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 03. 10. 2013.




WILAYA YA  MBEYA MJINI-    WATUHUMIWA  46  KATI YA  WATUHUMIWA 105
                                                              WALIOKAMATWA NA JESHI LA
                                                              POLISI MKOA  WA MBEYA KUTOKANA KWA 
                                                              TUHUMA YA  KUFANYA  VURUGU NA   
                                                              UHARIBIFU WAMEFIKISHWA
                                                             MAHAKAMANI LEO TAREHE 03.10.2013.

  • MNAMO TAREHE 03.10.2013 WATUHUMIWA 46 KATI YA  WATUHUMIWA 105 WALIOKAMATWA MAENEO YA  MWANJELWA,SOWETO,MAMA JOHN NA ILOMBA KWA TUHUMA ZA KUFANYA VURUGU WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KUJIBU MASHTAKA YANAYOWAKABILI YA KUFANYA FUJO/VURUGU NA UHARIBIFU WA MALI- BARABARA.

  • AWALI MNAMO TAREHE 02.10.2013 MAJIRA KATI YA  SAA 09:00HRS  HADI SAA 17:47HRS HUKO KATIKA MAENEO YA MWANJELWA, SOWETO, MAMA JOHN NA ILOMBA KUNDI LA VIJANA WAKOROFI NA WASIO  TAYARI KUTII SHERIA WALISHINIKIZA WAFANYABIASHA KUFUNGA BIASHARA ZAO NA KISHA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA  NA BARABARA ZA MITAA KWA KUWEKA MAWE MAKUBWA,  MAGOGO, KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KURUSHA OVYO MAWE KWA ASKARI POLISI HALI ILIYOSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA WANANCHI WA JIJI LA MBEYA KWA UJUMLA.

  • KUFUATIA VURUGU HIZO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA WANANCHI LILIKABILIANA NAZO NA KUFANIKIWA KUREJESHA HALI YA AMANI.

  • CHANZO CHA TUKIO HILI ILIKUWA NI WAHALIFU/WAFANYAFUJO KUTUMIA KIVULI CHA MALALAMIKO/MANUNG’UNIKO YA WAFANYABIASHARA KWENYE ENEO LA KODI HUSUSANI CHANGAMOTO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO KUWA BEI YA MASHINE YA KI-ELEKRONIKI NI GHALI  KIASI CHA TSH 800,000/= HIVYO WAO KUSHINDWA KUNUNUA.

  • HATA HIVYO KABLA YA VURUGU HIZO TAREHE 01.10.2013 WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 300 WALIPATA FURSA YA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA MHE ABBAS KANDORO WAKATI  WAFANYABIASHARA HAO WALIPOKUWA NA SEMINA ILIYOANDALIWA NA MAOFISA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MBEYA. KATIKA KIKAO HICHO WALIMUELEZA MKUU WA MKOA MANUNG’UNIKO WALIYOKUWA NAYO IKIWA NI PAMOJA NA BEI YA MASHINE YA ELEKRONIKI INAYOFANYA KAZI YA KUTOA RISITI KWA WATEJA NA KUWEKA KUMBUKUMBU.

  • JUMLA YA WATUHUMIWA 105 WALIKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MIONGONI MWAO WANAUME 103 NA WANAWAKE 2 KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI. AIDHA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA KWA WATUHUMIWA WENGINE 59 WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILO  IKIWA NI PAMOJA NA KUPEWA DHAMANA WAKATI UCHUNGUZI DHIDI YAO UKIENDELEA.

  • HAKUNA MADHARA MAKUBWA KWA BINADAMU AU MALI YALIYOTOKEA ISIPOKUWA UHARIBIFU WA KUCHOMA BARABARA.

  • KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI   ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA  WANANCHI NA WAKAZI WA MBEYA KUTOICHEZEA AMANI ILIYOPO KWANI  GHARAMA YA KUIRUDISHA NI KUBWA. AIDHA ANATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA KUENDELEA KUTAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO KWA KUJENGA HOJA KWA MISINGI YA KUTII SHERIA ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANAENDELEA KUTOA RAI YA KUENDELEA KUWAFICHUA WAHALIFU WAKIWEMO WAFANYA FUJO, VURUGU NA KUKATAA KUWAUNGA MKONO KATIKA MAOVU.


       

          WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                                   MIGUU NA  KUSABABISHA KIFO.

.
MNAMO TAREHE 02.10.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA HATWELO BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIACHA NJIA NA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 37-40 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. CHANZO NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.



                                                                        Signed by.
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




Previous
Next Post »