TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 27. 10. 2013.





WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 25.10.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPONA, KATA YA TOTOWE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. JAMPANY S/O MHAMALI, MIAKA 78, MNYIHA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MPONA ALIUAWA NA WATU WAWILI WASIOFAHAMIKA MAJINA AMBAO WALIMVAMIA NA KUMKATAKATA MAPANGA KICHWANI NA MKONO WAKE WA KULIA AKIWA NJIANI ANATOKA KWENYE KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA. MARA BAADA YA TUKIO HILO WANANCHI WA KIJIJI HICHO WALIANZA MSAKO MKALI KWA KUFUATILIA NYAYO ZA VIATU ZA WATUHUMIWA HAO NA KISHA KUWAKAMATA NDIPO WALIPOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KUWAUA KWA KUTUMIA SILAHA ZA JADI [MAWE]. KABLA YA MAUAJI HAYO WATUHUMIWA WALIKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA WALISEMA KUWA WALITUMWA NA MTU WALIYEMTAJA KWA JINA LA MANENO S/O ADAMSON @ LYAMBO. MTUHUMIWA AMETOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO, MSAKO MKALI UNAENDELEA ILI KUMKAMATA NA KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MWAMBANI - CHUNYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII. AIDHA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA KWENYE MAMLAKA HUSIKA. PIA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE ILI AKAMATWE.


WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 25.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA MAGAMBA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. ADELINA D/O PHILIMON, MIAKA 45,MNYAMWANGA, MKULIMA NA MKAZI WA MAGAMBA NA WASIWASI S/O MWASHIOMBO, MIAKA 28, MNYIHA, MKULIMA NA MKAZI WA IPOLOTO WILAYA YA MBOZI WALIUAWA KWA KUCHOMWA MOTO WAKIWA NDANI YA NYUMBA WAMELALA NA MTU AITWAE ZACHARIA S/O JOSEPH MWINGILA, MIAKA 39, MNGONI, MKULIMA, MKAZI WA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA. CHANZO CHA MAUAJI NI WIVU WA KIMAPENZI MARA BAADA YA KUMKUTA MPENZI WAKE AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. MIILI YA MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO.





Signed by:
[ROBERT MAYALA - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »