Hali hii imejitokeza baada ya wafanyabiashara kugoma kununua mashine za TRA ambayo thamani yake ni shilingi laki nane za kitanzania 800,000 hii imetokea Mbeya na Maduka yamefungwa kwahiyo hakuna bishara inayoendelea jambo ambalo pia linachangia kurudisha nyuma maendeleo.Naamini wahusika mtazungumza na wafanyabiashara ili kumaliza tofauti hizi na jambo hili lisijirudie tena. Nakumbuka mwaka juzi tarehe 11.11.2011 tukio kama hili lilitokea japo madai yalikuwa tofauti lakini hali ilikuwa hivi na maduka yalifungwa kwa siku 2 Tazama picha hapa chini
SATURDAY, NOVEMBER 12, 2011
VURUGU ZA WAMACHINGA MJINI MBEYA
Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na jiji la mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao |
Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao |
Wamachinga wakiwazomea polisi eneo la kabwe |
Maduka yote eneo la mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa |
Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya mbeya tunduma |
Huu ndiyo mtaa wengi huuita mtaa wa kasisi uliyosababisha vurugu zote kati ya wamachinga na askari wa jiji |
Mmachinga akiwarushia jiwe kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu |
Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana |
EmoticonEmoticon