HEBU ONA UNYAMA HUU MUME AMKATA MKE WAKE MGUU


aa_11477.jpg
bb_f747f.jpg

Na Waitara Meng'anyi, Tarime
Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

"Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati.
Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata alifiki kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.

" Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.

Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.
"Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa" alieleza .

Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.

" Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine ni baada ya kuoa mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu" alisema Ghati.

Ghati hataweza kurudiana na mume wake huyo kwa kitendo alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jera ili ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.

" Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula" alisema.

Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa na kukilaa kuwa kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .

" Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku kutuona sisi ni wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine" alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.

Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.

" Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema Kamugisha kwa nija ya simu
Previous
Next Post »