TYREES ASHINDA KESI YA MADAI YA KUWA HAMJALI MTOTO WAKE

   
  Mwanamuziki na mcheza Sinema  Tyres Gibson amefanikiwa kushinda kesi ambayo baby mama wake alimfungulia akidai kuongezewa malipo ya Child Support kwa madai kuwa Tyres hamjali mtoto wake.
 
  Lakini Tyres alileta ushahidi wa kuonyesha kuwa anamjali mtoto wake vilivyo ikiwa ni pamoja napicha ambazo zikionyesha jinsi anavyo utumia muda wake vizuri akiwa na mwanae,napia risiti za baadhi ya vitu vya thamani kubwa sana ambavyo huwa akimnunulia mtoto wake.
    Mbali na vitu hivyo Tyres pia alileta mashahidi ambao walisema kuwa Mwanamke huyo ni muongo kwani pamoja na Tyres kuwa busy sana na kazi huwa anutumia muda wake vizuri sana pale anapopata nafasi.
     Ushahidi wote huo ulimfanya Jaji kuitupilia kesi na kumpa Tyres ushindi ili kuwapa fundisho wanawake wanofungua kesi zisizo za msingi ili kujipatia hela kutoka kwa baby daddy zao.

www.swahilitv.info www.swahilitv.blogspot.com
Previous
Next Post »