TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 26. 09. 2013.






               
WILAYA YA  CHUNYA - MAUAJI.

MNAMO TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA  SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA NAMBINZO KATA YA NAMBINZO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MASOUD S/O JACKSON @ MWIVAVA, MIAKA 26, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA NAFCO - MAGAMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.  CHANZO NI BAADA YA MAREHEMU   KUPIGWA NA GONGO KICHWANI TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA  SAA 20:30HRS NA  ZAWADI S/O HAZOLE @ MKONDYA, MKAZI WA KIJIJI CHA MAGAMBA WAKATI MAREHEMU  AKIMDAI MTUHUMIWA PESA KIASI CHA TSHS 300/= ALIZOMKOPESHA WAKIWA KILABUNI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTU ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.



WILAYA YA RUNGWE -   WATUHUMIWA 34 WAMEFIKISHWA                                                    
                                                                                  MAHAKAMANI TAREHE
                                                                                  25.09.2013 NA JESHI LA
                                                                                  POLISI KWA KOSA LA KULA NJAMA
                                                                                  NA KUFANYA FUJO/KUFUNGA
                                                                                  BARABARA KUU MBEYA/TUKUYU KWA
                                                                                  MAWE NA MAGOGO.
                                                   
§  MNAMO TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA  SAA 15:35HRS HUKO KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA ILIYOPO  - TUKUYU MJINI WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. LAURENT S/O NICHOLAUS KASWAGA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBURA – KIWIRA NA WENZAKE 33 WALIFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA NA KUSOMEWA MASHTAKA MAWILI 1. KULA NJAMA NA 2. KUFANYA FUJO. AIDHA WATUHUMIWA WALISOMEWA MASHTAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA POLISI F.3644 D/C JOEL  MBELE YA  HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO MHE. MEBO MALAKASUKA.

§  KATIKA SHAURI HILO LA JINAI NO. 169/2013 WASHTAKIWA WOTE WAMEPELEKWA GEREZANI AMBAPO UAMUZI WA KUPEWA AU KUTOPEWA DHAMANA UTATOLEWA NA MAHAKAMA  TAREHE   09.10.2013.

§  AWALI MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI YA  SAA 18:00HRS HADI SAA 22:00HRS HUKO KATIKA KATA YA  KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA – KATI  NA KARASHA WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA BARABARA KUU YA  MBEYA/TUKUYU WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI YASIPITE NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO. THAMANI HALISI YA  UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO KUFAHAMIKA.

§  HATA HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA  TOYOTA L/CRUISER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI YA  MAREHEMU WATATU LILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA  TOYOTA COASTER NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI  NA UHARIBIFU KWA MAGARI YOTE MAWILI. CHANZO  CHA VURUGU HIZO  NI MADAI YA  KUONGEZEWA USHURU WA MAZAO [NDIZI] KUTOKA TSHS 100/=  ULIOANZA KUTUMIKA MWAKA 1989 NA KUFIKIA TSHS 200/= WAKISHINIKIZA URUDISHWE USHURU WA ZAMANI NA KUFUATIA VURUGU HIZO JUMLA YA  WATUHUMIWA 43 WALIKAMATWA.

§   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUWA CHANGAMOTO KATIKA JAMII HAZIWEZI KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO  KERO NA MAONI  YAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA NA KUKAA  MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI KWA KUZINGATIA HOJA.

§  AIDHA ANASISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI PIA KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE NA KWAMBA JESHI LA POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATU /KIKUNDI CHA WATU WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA  AMANI.KWA SASA HALI YA  ENEO HILO NI SALAMA.


WILAYA YA CHUNYA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                           MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA  MWAMBANI WILAYA YA  CHUNYA  MKOA WA MBEYA. GARI SM 9950 AINA YA  TOYOTA L/CRUISER MALI YA  HALMASHAURI YA  WILAYA YA  CHUNYA IDARA YA  UHASIBU ,LIKIENDESHWA NA DEREVA PHILIP S/O MANGULA, MIAKA 43, MHEHE, MKAZI WA SINJILI LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAGAKA S/O TINYA,  MIAKA 28, MSUKUMA ,MFUGAJI, MKAZI WA MAMBA – CHINI  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI BAADA YA  MTUHUMIWA KUJARIBU KUKIMBIA NA GARI KUFUATIA WAFUGAJI KUFANYA FUJO KWA KURUSHA MAWE BAADA YA  MIFUGO YAO KUKAMATWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA  CHUNYA - AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
                                                  KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA  SAA 17:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWAMBANI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. GARI T.721 ABG AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA MAIKO S/O PETER, MIAKA 37, KYUSA, MKAZI WA CHUNYA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA  LA YUSUPH S/O ? MIAKA 35, MSANGU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MTANILA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.




WILAYA YA  CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA  SAA 12:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA RAY S/O MICHAEL,  MIAKA 26, KYUSA, MKULIMA/BIASHARA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUPA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA  GRAM 500. MTUHUMIWA NI MUUZAJI  NA MVUTAJI WA BHANGI. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA SAA 09:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU  JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA NAPIL D/O PAUL, MIAKA 18, MUWEMBA , RAIA NA MKAZI WA NCHINI ZAMBIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO. AIDHA MAJIRA YA  SAA 12:00HRS ENEO HILO ALIKAMATWA PETHAS S/O TOBESES, MIAKA 24,RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA  ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.



Signed by:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.







Previous
Next Post »