NYONGEZA YA TAARIFA YA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE
26. 09. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MAGARI MANNE
KUGONGANA NA
KUSABABISHA VIFO. |
§
MNAMO
TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA
BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA KUELEKEA
DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON
S/O MACHA, AKIWA NA TINGO WAKE JUMA
S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO
KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
SAMWEL S/O ARON, MIAKA 30, MBENA, MKAZI
WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876
BKV/T.465 BQU AINA YA IVECO LORI
AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA PEMBENI YA
BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL S/O KASUSU, MIAKA 37, MJITA,
MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.
§
AIDHA
GARI HILO T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI,
MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA
KUUNGUA MOTO.
§
KATIKA AJALI HIYO MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX NA T.255
AKV/T.272 CDZ YOTE YAMEUNGUA VICHWA
NA KUTEKETEA NA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO
SEHEMU YA KICHWA UPANDE WA KULIA.
§
CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI
WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX.
§
MOTO
ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA
KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.
§
MIILI
YA MAREHEMU WILSON S/O MACHA NA JUMA S/O SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA KATIKA
GARI MWILI WA MAREHEMU SIXTUS S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA
MAGARI ENEO LA TUKIO ZINAENDELEA.
§
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed
By:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon