WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI
|
MNAMO
TAREHE 23.09.2013 MAJIRA YA SAA 09:30HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANYEGELE KATA YA
KIWIRA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. MTU
MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA
30-35 ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE. CHANZO
NI TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA WIZI WA PIKIPIKI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MAKANDANA RUNGWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE
WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA MOJA.
|
|
WILAYA YA CHUNYA -
KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 23.09.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA BWAWANI – MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA ALLY S/O DENIS MIAKA 26, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA BWAWANI AKIWA NA BHANGI KETE 10 SAWA NA UZITO WA GRAM
50. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon