WILAYA
YA MBARALI - MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 21/09/2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA WIMBA
MAHANGO WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. MARIAM
D/O NANIA, MSAFWA, MIAKA 47, MKULIMA NA MKAZI WA IJUMBI ALIOKOTWA AKIWA
AMEUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA KORONGO LA MTO BWIRI UKIWA
UMEHARIBIKA. MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE TANGU 15/09/2013 JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZILIFANYIKA MPAKA MWILI WA MAREHEMU ULIPOPATIKANA 21/09/2013. CHANZO
CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA AMBAPO KESI YAKE IPO KATIKA BARAZA LA
ARDHI KATI YAKE NA MTUHUMIWA ZUBERY S/O
YUSUPH, MIAKA 80, MZARAMO, MKAZI WA MAHANGO RUIWA NA WENZAKE WATATU (3) {1} MAWAZO S/O MAZINGA, MIAKA 53, MSAFWA, MKULIMA {2} JANGAMOHO S/O NANIA, MIAKA 48, MSAFWA,
MKULIMA NA {3}PILLY S/O NANIA, MIAKA
35, MSAFWA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA WIMBA MAHANGO AMBAO WAMETOROKA
MARA BAADA YA TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
WANANCHI/JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA. PIA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WATUHUMIWA HAO
AZITOE MARA MOJA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.
WILAYA YA CHUNYA –
KUPOATIKANA NA POMBE YA MOSHI {GONGO}
MNAMO
TAREHE 21/09/2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KIJIJI CHA MWAOGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.ASKARI
POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIWAKAMATA {1} MARY D/O MWAKATI, MIAKA 22, MNYAKYUSA, MKULIMA {2} ASNATI D/O FUNGAWASHENZI, MIAKA 23,
MNYAKYUSA, MKULIMA {3} RICHARD S/O
SIMON, MIAKA 25, MGURUKA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA CHUNYA WAKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI LITA KUMI NA TANO {15}.
WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUTUMIA
POMBEA HARAMU YA MOSHI {GONGO} KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
Signed by:
{DIWANI ATHUMANI – ACP}
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
EmoticonEmoticon