WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI – MTUHUMIWA MMOJA
AKAMATWA AKIUZA BIDHAA BANDIA POMBE KALI AINA YA KONYAGI.
MNAMO TAREHE 03/09/2013 MAJIRA YA SAA 12:45HRS
HUKO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO MAALUM KWA
KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA KAMPUNI YA
KONYAGI KUTOKA MAKAO MAKUU DSM WALIMKAMATA
ELIZA D/O SHIJA, MIAKA 28, MSUKUMA, MFANYABIASHA NA MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA ANAUZA POMBE
KALI AINA YA KONYAGI KATIKA DUKA LAKE
AMBAZO NI KATONI 117 YA CHUPA
NDOGO ZA KONYAGI NA DAZANI 9
YA KONYAGI MAARUFU KAMA VIROBA
AMBAZO NI BANDIA . THAMANI HALISI
YA BIDHAA HIZO BADO KUFAHAMIKA. TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA
KUACHA TABIA YA KUWA NA TAMAA YA KUJIPATIA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZISIZO
HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII HUSUSAN
WATUMIAJI WA VINYWAJI VYA AINA ZOTE KUWA MAKINI WANAPONUNUA BIDHAA HIZO KWANI
NYINGINE SIO SALAMA KWA MATUMIZI YA
BINADAMU NA PINDI WAKIWABAINI WATOE HARAKA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
ZINAZOHUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[ BARAKAEL
MASAKI - ACP ]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon