Mwanamke mmoja achomoka taya akipanua mdomo kung’ata ‘burger’.
Mwanamke
mmoja nchini Uingereza amelazimika kwenda hospitali kuunganishwa tena
taya yake baada ya taya hiyo kufyatuka mahali pake wakati akila ‘Burger’
ya vipande vitatu.
Mwanamke
huyo Nicola Peatekutoka Ormskirk, Lancashire alijiumiza mwenyewe wakati
akila mkate huo maarufu unaochanganywa na nyama, saladi na vitu vingine
katika mgahawa wa Almost Famous ulioko Liverpool.
Peate mwenye umri wa miaka 25 amesema kuanzia sasa atakuwa makini na ukubwa wa kitu anachokula.
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Idara ya Dharura ya Hospitali ya Royal Liverpool
University Kathryn Clark uchomokaji wa viungo wa aina hiyo hutokea mara
chache.
Peate
amesema katika siku zijazo kama chakula anachotaka kula ni kikubwa basi
ataomba kikatwe vipande vinavyowezekana kuingia mdomoni bila kuleta
madhara.
EmoticonEmoticon