TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 11. 08. 2013.


  WILAYA YA MBARALI – MAUAJI


MNAMO TAREHE 10.08.2013 MAJIRA YA  SAA 04:30HRS HUKO KIJIJI CHA MAPOGORO KATA YA MIYOMBWENI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA, MBUKE D/O OCHEGERI, MSUKUMA, MIAKA 34, MKULIMA NA MKAZI WA MAPOROGO ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU YA  KICHWANI NA KUNYONGWA  SHINGONI NA MUME WAKE AITWAYE NKUVA S/O MALALE, MIAKA 39, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MAPOGORO. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI AMBAPO MTUHUMIWA ALIKUWA ANAMTUHUMU MKEWE KUTEMBEA NA WANAUME WENGINE. MTHUMIWA AMEKAMATWA UCHUNGUZI UNAEDNELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE KUYATATUA MATATOZI YAO YA  KIFAMILIA KWA NJIA MBADALA YA  MAZUNGUMZO.



 WILAYA YA KYELA – WATUHUMIWA SITA WALIODHIBITIWA NA WAUMINI KWA USHIRIKIANO NA MAKACHERO WA POLISI KWA KUFANYA FUJO MSIKITINI WATAFIKISHWA  MAHAKAMANI KESHO  
                                            TAREHE 12.08.2013.


MNAMO TAREHE 12.08.2013  ASUBUHI WATUHUMIWA SITA WAUMINI WA DINI YA  KIISLAMU WALIOFANYA  FUJO KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA  KYELA NA KUDHIBITIWA WANATARAJIA KUFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA YA  KYELA NA KUSOMEWA MASHTAKA BAADA YA  TARATIBU ZA UPELELEZI KUKAMILIKA, MIONGONI MWA MASHITAKA HAYO NI PAMOJA NA  SHAMBULIO NA KUJERUHI.

AWALI MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO ENEO LA BONDENI KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. NURU S/O MWAFILANGO,MIAKA 77,KYUSA,SHEKHE MKUU WA WILAYA YA  KYELA, MKAZI WA BONDENI  AKIWA ANAONGOZA IBADA YA  SWALA YA    IDD EL FITRI  MSIKITINI HAPO ALIVAMIWA NA BAADHI YA  WAUMINI WANAOJIITA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUTUMIA FIMBO,NONDO,MKASI NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. CHANZO NI KUWA HAWAMTAKI SHEKHE HUYO KWA MADAI KUWA HANA UWEZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA WAKATI WAUMINI WOTE WAKIWA  WAMEINAMA WAKISWALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA. MHANGA HAKUPATA MADHARA BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKIANA NA POLISI/MAKACHERO WA KIISLAMU KUMUOKOA. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA SITA AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WALIKAMATWA AMBAO NI 1. MASHAKA S/O KHASIMU, MIAKA 30, MUHA, MKULIMA MKAZI WA NDANDALO 2. ISSA S/O JUMA, MIAKA 37, MRANGI, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI 3. AHMED S/O KHASIMU @ MAGOGO, MIAKA 35, MPOGORO, MKULIMA/MGANGA WA KIENYEJI, MKAZI WA MBUGANI [ALIKUTWA NA MKASI] 4. IBRAHIM S/O SHABAN, MIAKA 17, KYUSA, MWANAFUNZI SHULE YA  SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA NNE MKAZI WA NDANDALO [ALIKUTWA NA FIMBO KUBWA NA NDIYE ALIYEMNYANG’ANYA SHEKHE KIPAZA SAUTI] 5. AMBOKILE S/O MWANGOSI @ ALLY, MIAKA 19, KYUSA, MWANAFUNZI WA SHULE YA  SEKONDARI  KYELA DAY KIDATO CHA TATU, MKAZI WA BONDENI [ALIKUTWA NA KIPANDE CHA NONDO] NA 6. SADICK S/O ABDUL, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NDANDALO. AIDHA  KATIKA TUKIO HILO HAMIS S/O HUSSEIN, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI ALIPATA MAJERAHA KIDOGO KWA KUKATWA MKASI  JUU YA  SIKIO LA KUSHOTO WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMUOKOA MHANGA  ASIPATE MADHARA  NA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HALI YA USALAMA NA AMANI ILIREJEA MUDA MFUPI NA WAUMINI WALIENDELEA NA IBADA YAO CHINI YA UONGOZI WA SHEKHE HUYO NA KUMALIZA SALAMA. HAKUNA UHARIBIFU WA MALI ULIOTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAUMINI NA JAMII KWA UJUMLA KUTATUA MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA   KUKAA  KWENYE  MEZA YA  MAZUNGUMZO BAADA YA   KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANASISITIZA KUWA YEYOTE ATAKAYEJARIBU/ATAKAYEVUNJA SHERIA AWE NI KIONGOZI/MUUMINI WA DINI YEYOTE, AWE NI KIONGOZI WA SIASA, AWE NI MFANYABIASHARA N.K. HATAFUMBIWA MACHO.



signed buy

[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »