Mheshimiwa Dk. Hamis Kigwangalla akijibu swali kuhusu harakati za urais 2015 ndani ya CCM.
Fina Mango akimsiliza Mheshimiwa Kigwangalla wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi cha Makutano.
Mbunge
wa Nzega Mh. Dk. Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa
endapo jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais. Kigwangalla
aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Fina Mango katika
kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani
ya CCM juu ya mgombea urais huku Mheshimiwa Lowassa akiwa kati ya wale
wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.
“Sitompa kura Mheshimiwa
Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama changu
na nina hakika chama changu kikija na mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015
ambaye ana historia ya kuhusishwa
na mambo machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema wewe
mwenye hapa tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini
pia tutakuwa tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema kwamba tunalea
ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili” Alisema Mheshimiwa
Kigwangalla huku akiongezea kuwa Tanzania aihitaji rais asiyeweza
kusimamia ukweli.
Akijibu swali kuhusu
mitambo ya dowans, Kigwangalla alisema haoni tatizo la mitambo hiyo
isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake. Katika mahojiano
hayo Mheshimiwa Kigwangalla alitangaza nia yake ya kugombea urais mwaka
2025 na kuongezea kuwa 2015 anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini
watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa aina gani.
EmoticonEmoticon