Taarifa toka Morogoro zinaarifu kwamba Sheikh Ponda amepigwa risasi na polisi baada ya wafuasi wake kuandamana.....
Taarifa hizo zinaeleza kwamba Sheikh Ponda alikuwa akiendesha mhadhara mkoani Morogoro.Baada ya mhadhara huo, wananchi walianza kuandamana kuelekea barabarani ambapo polisi walijitokeza kukabiliana nao....
Ponda anadaiwa kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo na haijulikani hali yake kwa sasa....
Hata hivyo , kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amekanusha madai hayo ya kupigwa risasi na kueleza kuwa hali ni shwari mkoani Morogoro kwa sasa baada ya machafuko ya muda mfupi mida ya jioni....
Akizungumzia kuhusu Ponda, Shilogile amesema kuwa yeye hajui hali yake maana polisi walizuia gari lake ili wamkamate kwa tuhuma za uchochezi zinazomkabili, lakini wananchi wakaanza kuwashambulia polisi na wakafanikiwa kumtorosha....
Baada ya shambulio hilo, Polisi walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya wananchi .
Shilogile anatoa wito kwa mtu yeyote anayejua alipo Ponda awaarifu polisi mapema
Source:MPEKUZI
EmoticonEmoticon