
Sherehe za kuapishwa kwake zimekuwa
zikicheleweshwa kwa sababu ya kesi iliyokuwa imewasilishwa mahakamani
kupinga kuchaguliwa kwake na mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai ,
ambaye alidai kulikuwa na wizi wa kura.Tsvangirai pia anadai wapiga kura
wake milioni waliondolewa kwenye vituo vya kupigia kura katika maeneo
ya mijini , yanayoaminiwa kuwa ngome yake ya kisiasa.
Itakuwa ni fursa nyingine kwa rais
Robert Mugabe kutoa hotuba zake zenye makali hususan kuyashutumu mataifa
ya magaribi kutokana na vikwazo vilivyowekewa zimbabwe na kuuponda
upinzani unaoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Morgan Changirai.
Ni nafuu iliyoeje kwa bwana Mugabe
ambaye alilazimika kugawana madaraka na bwana Changirai kwa kipindi cha
miaka mitano iliyopita kufahamu kuwa mara hii atakuwa ni yeye pekee
kwenye usukani wa kuiongoza zimbabwe.
Zaidi ya marais arobaini wa mataifa ya
kigeni wamealikwa katika sherehe za leo lakini haijabainika ni wangapi
watahudhuria kushuhudia kuapishwa kwa Robert Mugabe katika uwanja mkubwa
zaidi wa michezo nchini Zimbabwe mjini Harare. Leo Alhamisi imetangazwa
kuwa siku ya alhamisi ili kuwaruhusu wafuasi wa rais huyo mkongwe
kuhudhuria sherehe hizo.
Waandalizi wamesema kuwa sherehe za
leo zinatarajiwa kuwa za hali ya juu kuliko sherehe za mwaka 1980 baada
ya Zimbabwe kunyakuwa uhuru.
Hatua hii inalenga kuwashawishi raia
kwamba uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa haki baada ya shutuma kwamba
kulikuwa na udanganyifu na wizi wa kura.
Mpinzani mkuu wa bwana Mugabe Morgan
Tsvangirai alipuuzilia mbali uchaguzi huo, akiutaja kuwa bandia na ambao
haukuashirii matakwa ya watu wa Zimbabwe. Bwana Changirai ametaka
kufanyiwa ukaguzi daftari la kudumu la wapiga kura.
Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe
ilitangaza kuwa chama cha Zanu PF kilishinda thuluthi tatu ya idadi ya
viti bungeni na kwamba Mugabe alinyakuwa ushindi wa zaidi ya asilimia
sitini ya kura zilizopigwa. Chama cha MDC chake Morgan Changirai
kimesema kuwa hatahudhuria sherehe za leo.
EmoticonEmoticon