Waziri
wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawambwa akifafanua
jambo wakati akizindua wa utekelezaji wa mikakati ya “Matokeo makubwa
Sasa” ambapo kwa kingereza unaitwa “Big Result now” katika sekta ya
elimu. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi mpya wa mwalimu Nyerere
jijini Dar es salaam, mpango huu utaongeza fursa za ukuaji Uchumi
Wananchi na kuchochea Ustawi kwa Maisha bora kwa Watanzania wote.
Maafisa
wa Elimu mikoa wakitoa ahadi zao kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya
ufundi Mhe. Dk. Shukuru Kawambwa namna watakavyoenda kutekeleza mpango
wa “Matokeo Makubwa Sasa”katika sehemu zao za kazi.
Baadhi
maafisa wa Elimu mikoa wakisaini nakala za ahadi za mpango huo(wa
kwanza kulia)Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Bw.Hirson Kipenya ,akifuatiwa na
Yusufu Kipengele Mkoa wa Pwani, Ibrahim Mbango, Mkoa wa Manyara
wanaoshuhudia (wa kwanza kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi
Mhe. Dk Shukuru Kawambwa (katikati) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Philipo Mulugo(wa kwanza kushoto)Naibu waziri wa Tamisemi Mhe,
Naibu Waziri wa Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa.
Wadau
wa Elimu wakiwa kwenye mkutano huo wakati wa uzinduzi wa “Matokeo
makubwa Sasa” ambapo kwa Kiingereza unaitwa “Big Result now”kwa sekta ya
Elimu.
Kikundi cha ngoma Parapanda kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.
EmoticonEmoticon