Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike
wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa
kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja
na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa
maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana
ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa
Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze
kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum
Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi
Catherine Mashalla.
Katika
kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama
cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim
mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi
wanapouhitaji. Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa
wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo
yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni
mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana
kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi
walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia
nyingine kiuchumi.
Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika
kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo
rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za
namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na
badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.
Mkuu
wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali
wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na
maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia
mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya
madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary
Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza
kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya.
EmoticonEmoticon