TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 1.
Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na
Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu
(Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016 2.
Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya
taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha
kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya
Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani
na Azam Media. Kwa kuwa wawazi,
Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA
kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana
sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya
mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila
haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom
Premier League katika Azam Television. Sote
tumeona baada ya hapo kuwa "nguvu ya ziada" inatumika kupotosha msimamo
wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA
hadharani. Juu ya hayo Na Kwa
kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa
kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu
wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya
Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa
vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu
zinazojionyesha wazi. Inadhihirika
wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama
kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television. Kwa
kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi
yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana
na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa
Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya
Klabu yetu. Kwa kuzingatia hali
hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA,
natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti,
2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30
asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha
mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI) MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
DIAMOND AKODISHA PRIVATE JET BAADA YA KUKWAMA NAIROBI
Baada ya kukwama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jommo Kenyatta,
Msanii machachari hapa nchi anae sifika kwa kua na pesa nyingi
amekodishiwa ndege binafsi na kampuni ya coca cola..
Diamond Plutnumz ni balozi wa coca cola.....
Diamond aliweka katika mtandao wa instagram na kuweka maneno haya
Had no choice than dat coz I miss my mum and baby lyk crazy.... @Wilson Airport Nairobi...I cant wait to see you #rammyjones #myself#AloneInTheJet#coca boy.....#coca cola mmetisha sana asanteni sana
- See more at: http://williammalecela.blogspot.com/2013/08/diamond-akodisha-private-jet-baada-ya.html#sthash.ipLIxIfC.dpuf
EmoticonEmoticon