Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella
Mukangara akizungumza na Viongozi wa Steps Entertainment (hawako
pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya
maendeleo ya kazi za sanaa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri akitoa darasa kwa baadhi ya washiriki waliohudhuria kikao.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo akichangia wakati wa kikao
kati ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt.
Fenella Mukangara na Steps Entertainment.
Moja
ya viongozi wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Damodaran akifafanua
jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
Baadhi
ya viongozi walioshiriki katika kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara
(hayupo pichani) wakati akiwaelezea jambo wakati wa kikao jijini Dar es
Salaam.
Mtaalum
Mshauri Bw. Sanctus Mtsimbe akiomuonyesha Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) moja
ya kazi yake iliyopitia taratibu zote na ambayo hakimiliki ni yake
mwenyewe.
Kushoto
ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamun Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa
Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko wakisikiliza majadiliano wakati wa
mazungumzo kati ya Steps na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi wa Steps wakimsikiliza Katibu wa Bodi wakati akielezea
jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Mhe. Dkt. Fenella Mukangara kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
WAZIRI
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
amekutana na wadau wa Kampuni ya Steps Entertainment na kuzungumza nao
juu ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini. Ujumbe huo wa Steps
ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki
Katika
mazungumzo hayo Dkt. Fenella amegusia masuala ya uharamia katika kazi
za filamu nchini na kutia mkazo katika suala zima la maadili. Aidha
Waziri ameeleza kuwa kuanza kwa urasimishwaji wa tasnia ya filamu na
muziki unaoendelea kutekelezwa nchini kutasaidia sana kuondosha kazi
zisizohalali.
Aidha,
Dkt. Fenella amewashauri wadau wa tasnia ya filamu nchini washirikiane
kikamilifu na Serikali katika kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na
pia kuhakikisha wasanii wananufaika na jasho lao. Aidha ameeleza umuhimu
wa kutoa elimu kwa wadau na umma kwa ujumla juu ya fursa nyingi
zilizopo katika tasnia.
Kwa
upande mwingine Waziri Dkt. Fenella ameshauri pia kuwe na majumba
maalum kwa ajili ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa
kipaumbele filamu za kitanzania pia amehamasisha wadau wa filamu
kuanzisha majumba hayo na ambao tayari wameanzisha kutoa fursa hiyo ili
kuziendeleza kazi za filamu za kitanzania.
“Kuwe na majumba ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania”. Alisema Dkt. Fenella.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo
alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la filamu zinazowasilishwa
kwa ukaguzi na pia wadau wameanza kutumia stempu za TRA katika kazi za
filamu na muziki ili kuzilinda kazi hizo. Stampu zilianza kutolewa tangu
mwezi Januari mwaka huu .
Kwa
upande mwingine Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki wa Kampuni ya Steps
Entertainment ameiahidi Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana na
Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Mukangara, kuendelea kuendeleza tasnia ya
filamu kwa kushirikiana kikamilifu na serikali na kupiga vita uharamia
dhidi ya filamu za kitanzania . Aidha wameiomba serikali kuendelea
kuwajengea mazingira mazuri.
EmoticonEmoticon