Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ruvuma na Wilayani Tunduru


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mkulima stadi  wa Namtumbo, Bosco Luambano ambaye alimzawadia Waziri Mkuu mikungu miwili ya ndizi katika mkutano wa hadhara  katika mji mdogo wa Namtumbo. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
 Waziri  Mkuu Mizengo Pinda akiwashukuru wazee wa Mji Mdogo wa Namtumbo bada ya kutawazwa kuwa moja wa wazee wa mji huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo  Julai 16, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa machinjio ya kisasa katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 16, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizundua  mitambo ya kuzalisha umeme katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 16, 2013. Kushoto ni Naibu Wairi wa Nishati na Madini Stephen Masele.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (kushoto) wakisalimiana na Mkurugenzi wa  Kanisa la  Upendo wa Kristo Masihi  (KIUMA), Dr. Matomola Matola  (wapili kuli) baada ya kuwasili katika misheni hiyo kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Elimu cha Misheni hiyo, Julai 15, 2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Chuo cha Elimu cha Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA) wilayani Tunduru akiwa katika iara ya mkoa wa Ruvuma Julai 15,2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza maswali kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Tunduru katika mkutano wa hadhara aliohutubia kwenye uwanja wa michezo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 15, 2013.
 Mmoja wa wananchi wa Tunduru akimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pindawakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Tunduaru  akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 15, 2013.
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akizungumza  kabla ya kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Elimu cha Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA) wilayani Tunduru akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 15, 2013.
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mkrugenzi wa Kanisa la Upendo  wa Kristo Masihi , Dr. Matomola Matomola kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Chuocha Elimu cha Kanisa hilo wilayni Tunduru akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wazee wa Tunduru kwenye Ikulu ndogo ya Tunduru akiwa katika ziara ya mkoa wa Ryvuma Julai 15, 2013.  Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Thabiti Mwambungu.Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu
Previous
Next Post »