Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Said Mwema, akimkabidhi zawadi yenye nembo ya Jeshi Polisi Tanzania,
Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan,
jimbo la Darfur, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es salaam, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku sita
hapa nchini.
Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed
Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur (wapili kutoka
kulia), akitoa mada katika kikao cha kubadilishana uzoefu
kilichowashirikisha makamishina na maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi
Nchini. Kutoka kulia ni Kamishina wa utawala na fedha wa jeshi la
polisi, CP Clodwig Mtweve, Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi
la Polisi, CP Paul Chagonja, Mkuu wa tathmini na ufuatiliaji Naibu
Kamishina wa Polisi (DCP) Omar Rashid pamoja na Mkuu wa Utawala na
rasilimali wa jeshi la Polisi (DCP)Thobias Andengenye.
EmoticonEmoticon