VYETI VYA SHULE YA MSINGI VYAONESHA FALCAO NI MKUBWA ZAIDI ANAYOSEMA


falcao a2d45
Profile ya Falcao inayonyesha na umri wa miaka 27 wakati ni 29 (HM)

Wakati masuala ya wachezaji wa soka kufoji vyeti vya kuzaliwa kuficha umri wao halisi ukiwa umewaandama wachezaji wa kiafrika, leo hii zimeibuka ripoti kutoka Amerika ya Kusini zikiripoti kwamba mshambuliaji wa kikorombia Radamel Falcao amefoji umri wake.

Kwa mujibu wa vyeti vyake vya shule ya msingi vinaonyesha nyota huyo wa Monaco amezaliwa mwaka 1984 na sio 1986 kama inavyoonekana kwenye wasifu wake. Falcao alianza kusoma kwenye shule ya msingi ya Colegio San Pedro Claver iliyopo kwenye mji wa Bucaramanga akiwa na miaka mitano mnamo mwaka 1989. 

Kwa maana hiyo Falcao amejipunguzia umri wa miaka 2 katika umri wake wa halisi ambao ni miaka 29 mpaka sasa. Tangu kuanza kusambaa kwa taarifa hizi sio mwenyewe mchezaji wala wakala wake ambaye ajitokeza hadharani na kukanusha.

 Chanzo: shaffihdauda
Previous
Next Post »