Kucheua
kwa mtoto ni hali ya mtoto kutoa chakula kupitia mdomoni muda mfupi
baada ya kula/kunyonya.Kucheua kwa mtoto hupungua kadri mtoto anavyokuwa
mkubwa na ni nadra sana kutokea baada ya mtoto kufikisha umri wa miezi
18.
Kucheua pia kunaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi kwa mtoto kama ugonjwa wa Gastro-esophageal Reflux Disease (GERD), mzio (allergy) au kuziba kwa mrija wa kupitishia chakula.
Nini husababisha mtoto kucheua baada ya kula?
a) Maumbile ya asili ya misuli ya mtoto (lower oesophageal sphincter)-Kwa watoto wachanga, misuli inayounganisha mrija wa kupitisha chakula na tumbo yaani lower oesophageal sphincter, huwa haijakomaa (immature),hivyo
kuruhusu chakula (maziwa) kurudi juu yaani kuelekea mdomoni badala ya
kwenda kwenye tumbo moja kwa moja.Kazi maalum ya misuli hii ni kufungua
njia kuruhusu chakula kuingia kwenye tumbo na kufunga kuzuia chakula
kurudi kilikotoka yaani mdomoni.Hivyo, kutokukomaa kwa misuli hii
huchangia kucheua kwa watoto
b)
Maziwa ya watoto pia huchangia kutokea kwa hali hii kwani maziwa yapo
kwenye majimaji hivyo ni rahisi kurudi juu na kutolewa tena mdomoni.
c)
Kuwepo kwa hewa kwenye tumbo ambayo hutokana na mtoto kunyonya haraka
sana/kunyonya sana au mama kutojuwa jinsi ya kumnyonyesha mtoto wake kwa
njia sahihi huchangia kutokea kwa hali hii ya kucheua.
Kwa kawaida mtoto hucheua baada ya kunyonya lakini mara nyingine kucheua kwa mtoto hutokana na;
I. Allergic gastroenteritis- Mzio (Allergy) wa protini inayopatikana kwenye maziwa ya ng’ombe
II.
Gastroesophageal reflux disease (GERD)-Huu ni ugonjwa unaosababishwa na
kucheua kwa tindikali inayotoka tumboni ambayo pia huharibu kuta za
mrija wa kupitisha chakula (oesophagus).Kitu chochote kile kinachoongeza
presha (Intra-abdominal pressure) chini ya lower oesophageal sphincter kama uzito ulopitiliza (obesity), kutopata choo kwa muda (constipation), baadhi ya vyakula, vinywaji na baadhi ya dawa husababisha GERD.
III.
Eosinophilic oesophagitis- Hali inayotokana na kukusanyika kwa wingi kwa
chembechembe za damu aina ya eosinophils na hivyo kuharibu kuta za
mrija wa kupitisha chakula.
IV.
Mrija wa chakula kuwa mwembamba/kuziba hali inayojulikana kitaalamu kama
oesophageal stricture au sehemu ya misuli kati ya tumbo na mrija wa
chakula kuwa nyembamba au kuziba nayo hujulikana kwa kitaalamu kama
pyloric stenosis
Dalili za Infant Reflux
Kucheua kwa mtoto ni hali ya mabaki ya chakula kutolewa kupitia mdomoni baada tu ya mtoto kunyonya.Mtoto pia anaweza kutapika. Ikiwa mtoto wako ana afya njema, hana tatizo basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kama akicheua au kutapika baada ya kunyonya ingawa kabla ya kupata hali hii mtoto anakuwa anasumbuka sana au kulia, akiashiria kupata taabu tumboni kwa sababu hajacheua/kutapika, hivyo wewe kama mama au baba hutakiwi kuwa na hofu.
Ni wakati gani wa kumpeleka mtoto kwa daktari?
Mpeleke mtoto kwa daktari kama;
I. Haongezeki uzito
II. Anacheua kwa nguvu mpaka macheuo au matapishi yakaruka nje kwa nguvu sana (projectile vomiting)
III. Anajikamua sana kabla ya kucheua/kutapika na kupata maumivu
IV. Anacheua macheuo ya rangi ya kijani au ya njano
V. Anacheua macheuo yaliyochanganyika na damu au yenye rangi ya kahawia
VI. Anakataa kunyonya
VII. Anapata choo kilichoambatana na damu
VIII. Anapumua kwa shida
IX. Anatapika baada ya kufikisha miezi sita
X.
Anapata taabu ya kumeza chakula,kunguruma kwa sauti yake (hoarseness of
voice),ana maumivu ya koo (sore throat), pua zimeziba kwa muda mrefu,
maambukizi kwenye pua/masikio
Kama mzazi tambua ya kwamba;
a)
Baadhi ya watoto huanza kucheua wakati meno yanapoanza kuota, wakati
wanaanza kutambaa,au wakati wanaanza kula vyakula vigumu (solid foods).
b)
Baadhi ya watoto wakati wa kunyonya hutoa titi la mama ili waangalie
mazingira yanayowazunguka/au wale wanaopenda kucheza na titi la mama
wakati wa kunyonya,huingiza hewa ndani na hivyo kusababisha kucheua
c) Kucheua hutokea baada tu ya mtoto kunyonya au saa 1-2 baada ya kunyonya
d) Watoto wachanga hadi kufikia umri wa miezi mitatu hucheua angalau mara moja kwa siku
e) Kucheua kwa watoto huongezeka mtoto anapofikisha umri wa miezi 2-4
f) Watoto wengi hupunguza kucheua wanapofikisha umri wa miezi 7-8 na
g) Huacha kabisa wanapofikisha umri wa mwaka mmoja
Vipimo vya Uchunguzi
Kama
daktari wako atahisi mtoto wako ana tatizo zaidi kutokana na hali yake
ya kucheua, baadhi ya vipimo ambavyo anaweza kumfanyia mtoto ni kama
ifuatavyo;
I.
Ultrasound-Kipimo hiki kinaweza kuonyesha kuziba/kupungua kwa njia ya
mrija wa chakula au kama mtoto ana pyloric stenosis kama nilivyoeleza
hapo awali
II.
Vipimo vya damu kama Complete blood Count ambacho huangalia wingi wa
chembechembe za damu, maumbile yao, aina ya chembechembe hizo. Pia
kipimo cha mkojo (urinalysis) ni muhimu kufanywa.
III.
Eosophageal PH monitoring- Kipimo hiki husaidia kujua kama macheuo ya
mtoto yana tindikali au la na hufanywa kwa daktari kuingiza mpira
mwembamba kupitia pua au mdomo wa mtoto mojamoja kwenda kwenye mrija wa
chakula, mbele ya mpira huu kuna kifaa maalum cha kupima PH ya mtoto
wako kwa ndani.Kipimo hiki pia kitamsaidia mzazi kujua kama malalamiko,
usingizi wa taabu anaopata mtoto (sleep disturbance) na mtoto kulia mara kwa mara (irritability) hutokana na tindikali au la.
IV.
X-rays za tumbo (Upper GI Series- Mtoto hupewa dawa kama chaki ya
majimaji na kisha hupigwa picha za X-rays ambazo zitaonesha kama kwenye
utumbo wa mtoto ana shida yoyote ile.
V. Upper
endoscopy-Kipimo hiki ambacho hufanywa kwa kutumia mpira maalum wenye
kamera kwa mbele ambao huingizwa kwenye mrija wa chakula (oesophagus)
kupitia mdomoni mpaka kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo na kwenye
tumbo, husaidia kujua kama mrija wa chakula umeziba/kuwa mwembamba au
umepata mcharuko wa maambukizi (oesophagitis).Kipimo hiki kwa watoto hufanywa kwa mtoto kupewa dawa ya usingizi au nusu kaputi.
Matibabu ya kucheua
Mara nyingi kucheua kwa mtoto hakuna madhara yoyote yale na husaidiwa kwa;
I.Kumpa mtoto milo midogo midogo mara nyingi (small frequent feedings)
II.Kukatisha chakula na kumweka mtoto begani
III.Kumweka/Kumshika mtoto akiwa wima wakati wa kunyonya au baada ya kunyonya
IV.Hakikisha unamlaza mtoto chali na si kulala kifudifudi
V.Tiba inaweza kuwa ya dawa kama ambazo zinazozuia tindikali au ya upasuaji (fundalplication procedure) kwa wale wenye pyloric stenosis.
EmoticonEmoticon