“PRESS RELEASE”
TAREHE 08. 07. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI
- MAUAJI
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA USIKU HUKO MTAA WA MBATA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ODEN S/O MKUMBWA, MIAKA 60, MNDALI, MLINZI BINAFSI MKAZI
WA NONDE ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA KAZINI KATIKA LINDO AMBALO NI DUKA LA MADAWA
MUHUMU [PHAMACY] LILILOPO ENEO HILO. MBINU ILIYOTUMIKA NI WATUHUMIWA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA KATIKA
LINDO NA KUMUUA KISHA KUVUNJA DUKA HILO
LA DAWA MUHIMU NA KUIBA DAWA ZA AINA
MBALIMBALI PAMOJA NA FEDHA TASLIMU TSHS 600,000/=. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MAHALI WALIPO WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE.
WILAYA YA RUNGWE -
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO ILIMA
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.654 BPX AINA
YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA
IMANI S/O MWAKILEMA,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
MAGE D/O NSUKEMO,MIAKA 59,KYUSA,MKULIMA ,MKAZI WA ILIMA NA KUMSABABISHIA KIFO
CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA
HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU KWA
AJILI YA MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA ILEJE -
AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA VIFO.
KUSABABISHA VIFO.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MBEBE WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA
LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI T. 863 BXC AINA YA SANYA AITWAE OBADIA S/O MWAKIPESILE,MIAKA
36,KYUSA,MKAZI WA MBEBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE FRED S/O FUMBIKA,MIAKA
23,MNDALI,FUNDI UJENZI MKAZI WA ISANGA MBEYA NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO
HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MIILI
YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI YA
WILAYA YA ILEJE. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO .KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI. ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI -
ACP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon