Binti mmoja nchini Afrika Kusini amenusurika kifo baada ya kumbusu simba anayefugwa aliyekuwa amefungiwa katika banda lake katika hifadhi ya wanyamapori nchini humo.
Kijana huyo Lauren Fagen kutoka Montreal amepata majeraha kadhaa mwilini kwake wakati Simba huyo dume alipovuta miguu yake ndani ya banda hilo katika kituo cha Moholoholo Wildlife Rehabilitation.
Lauren Fagen akiwa Hospitalini akiuguza majeraha baada ya kujeruhiwa na Simba huyo.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 18 anayefanya kazi za kujitolea anaye endelea na matibabu katika hospitali amesema ni bahati kubwa kwake kuwa hai.
Fagen alianza kazi za kujitolea katika kituo cha wanyamapori mwezi Juni mwaka huu akifanya usafi katika mabanda ya simba na kuwalisha wanyama wengine.
EmoticonEmoticon