WANAMUZIKI wa kike watatu maarufu Pauline Zongo, Khadija Mnoga, pamoja na Joan Matovolwa wameungana na kuunda kundi jipya linaloitwa 'Ndege watatu' na kutoa nyimbo inayojulikana kwa jina la Misukosuko.
Wanamuziki hao ambao wameamua kuja kwa mtindo tofauti kwa kutoa nyimbo hiyo kwa kutumia lugha tatu tofauti ikiwemo Kiswahili, Kilingala pamoja na Kingereza.
Wasanii hao ambao wameamua kutumia lugha hizo kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wao mbalimbali wakiwemo hata wale wasiojua lugha ya kiswahili.
Wasanii hao ambao kila mmoja alikuwa akijishughurisha na maswala ya muziki kwa kipindi kirefu akiwemo Paul Zongo mwenye asili ya Kikongo wameamua kurudi katika gemu hilo kwa kuunda kundi ikiwa ni kuhamasisha wanawake kujiingiza katika maswala ya muziki.
Kundi hilo ni miongoni mwa kundi linaloundwa na wanawake watatu wenye lengo la kukuza muziki nchini Tanzania.
EmoticonEmoticon