“PRESS RELEASE”
TAREHE 30. 07. 2013.
WILAYA YA RUNGWE –
MAUAJI
MNAMO
TAREHE 29.07.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IJOKA KATA YA
MPOMBO WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. JANETH
D/O BENISON MWAILIMA, MIAKA 6, MNYAKYUSA NA MKAZI WA KIJIJI HAPO. ALIUAWA KWA
KUKATWA NA PANGA SHINGONI NA KWENYE MKONO WAKE WA KULIA NA MTUHUMIWA NARBETH S/O HAULE, MIAKA
14, MNGONI, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA IJOKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KUPOTEZA
USHAHIDI BAADA YA MTUHUMIWA KUMBAKA MAREHEMU NA KISHA KUMUUWA. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA/KUDHIBITI TAMAA ZA KIMWILI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MADHARA ENDAPO
HAZITADHIBITIWA.
Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon