TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



  


PRESS RELEASE” TAREHE 24. 07.2013.

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI [MATAIRI KUUNGUA MOTO]

MNAMO TAREHE 23/07/2013 MAJIRA YA SAA 14:00 HRS HUKO ENEO LA MACHIMBO BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA MBEYA. GARI NO. 9154 AA 19 TRELA NO 4817AB 19 LIKIENDESHWA NA DEREVA EDSON S/O SIVIAN, MIAKA 40, MDIGO, MKAZI WA DSM LIKITOKEA DSM KWENDA CONGO LIKIWA LIMEBEBA MAFUTA YA PETROL, MATAIRI YA NYUMA YALIJAM NA KUWAKA MOTO AMBAO ULIFANIKIWA KUZIMWA .  HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI NA KUVIFANYIA UKAGUZI WA MARA KWA MARA VYOMBO  HIVYO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.  



Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.














Previous
Next Post »