THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete atoa maelekezo kuhusu kodi ya simu za mkononi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi
na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara
moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo
za mikononi.
Rais kikwete ametoa maelekezo hayo
jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara
ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa
makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha
pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la
mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe
ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea
katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi
italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa
Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa
pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta
njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo
tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni
bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza
pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha
wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,”
Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka
2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji
simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
EmoticonEmoticon