Mmoja wa waimbaji maarufu wanaofahamika nchini Zimbabwe Chiwoniso Maraire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 37.
Albam aliyoitoa Chiwoniso iliyoitwa ‘Ancient Voices’ ilimfanya kuwa staa katika dunia ya muziki katika miaka ya 1990.
Alikuwa
akipiga ‘mbira’ au ‘thumb piano’ chombo ambacho nchini humo ni wanaume
tu pekee kitamaduni ndio waliokuwa wakitakiwa kukipiga.
Amefariki
kwa kile kunachihisiwa kuwa ni ugonjwa wa Nimonia, ikiwa ni mwaka mmoja
tu tangu kifo cha aliyekuwa mume wake Andy Brown, ambaye pia alikuwa
mwanamuziki mahiri.
Wanandoa hao wa zamani wameacha watoto wawili.
Chiwoniso
alikuwa binti wa mwanamuziki anayeheshimika Zimbabwe kwa kupiga ‘Mbira’
Dumisani Maraire, aliyefundisha katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe.
Hakupata
tu heshima kwa kuwa alivunja mwiko kwa kupiga ‘mbira’ lakini pia kwa
kufanikiwa kuuchanganya sauti za asili za Zimbabwe na vyombo vya kisasa.
Alizaliwa marekani mwaka 1976 na baadae kurejea nchini kwao Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 7.
EmoticonEmoticon