Jamaa za familia ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,  wamewasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya mjukuu wa Mandela,Mandla Mandela.
 Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama  watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla  za kufukua makaburi kinyume na  sheria
 Mwendesha mashtaka wa umma, kisha ataamua ikiwa amshtaki Mandla au la.
 Inahusisha maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na  Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita.
 Katika  kesi nyingine, jamaa kumi na sita wa familia ya Mandela, wanataka  kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye  anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
 Kesi hiyo  inayosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki  iliakhirishwa hapo jana kuanza kusikilizwa leo.
 Wiki jana, mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa  kutoka nyumbani kwa Mandla katika kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa  kilomiya 22.
 Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.
 
 
EmoticonEmoticon