Mbunge
wa Arusha mjini Mh.Godbless Lema leo amefikishwa katika mahakama kuu
kanda ya Arusha kwa kosa linalomkabili la kutoa maneno ya uchochezi kwa
mkuu wa mkoa Arusha,tukio lililo tokea mnamo tarehe 24 mwezi wa Aprili
katika chuo cha uhasibu Njiro ambapo wanafunzi hao walikuwa
wamekusanyika katika eneo hilo wakitaka kuonana mkuu wa mkoa pamoja na
RPC ili kuzungumzia usalama chuoni hapo.
Akisomewa
shitaka hilo mahakamani hapo ,wakili wa serikali Bi. Elianeny Njiro
amesema mstakiwa Lema alifika chuoni hapo siku ya tukio na kuongea
maneno kwa kutumia lugha ya uchochezi kwamba ‘amekuja kama anakwenda
kwenye sendoff kauli hiyo ilichochea vurugu kwa wanafunzi kwa kupelekea
wanafunzi hao kurusha mawe, chupa, wakati huo mkuu wa mkoa alipokuwa
akitoa hotuba ,hali hiyo ilipelekea uvunjifu wa amani.
Aidha
tukio hilo linatokana na mauaji ya mwanafunazi Henry Koga aliyefariki
23/4 kwa kuchomwa kisu na watu wasiofahamika na liliripotiwa polisi
ambapo polisi waliweza kufika eneo la tukio kwa na kufanya upelelezi
upelelezi ambapo upelezi huo uliendelea na mshtakiwa kufikishwa
mahakamani katika maelezo hayo wakili wa mshtakiwa bwana Method
Kimomogoro alisema maelezo yanayokubalika na kwamba mshtakiwa tarehe
24/4/2013 alikuwepo chuoni hapo lakini maneno yaliyosalia kwamba alitoa
maneno ya uchochezi sio ya kweli.
Hakimu
aliyeendesha kesi Bi Devota Msofe alisema shauri la kesi hiyo litatajwa
kwa siku tatu mfululizo ambazo ni tarehe 20,21,22 mwezi wa nane huku
kukiwa na mashahidi kwa upande wa serikali ambao ni SSP Gilles Muloto wa
polisi arusha, Inspecta Jane mkaguzi wa polisi arusha ,inspeta Benard
nyambanya,PC Godfrey johachimu Wiliamu mahanyi wa polisi, Faraji kasidi
wa chuo cha uhasibu njiro ,John Joseph wa chuo cha uhasibu
njiro,Benjamini simkanga wa chuo, na naibu hamidu, hata hivyo mahakama
iliridhia na shauri lililotajwa pamoja na mashahidi na dhamana kwa
mshtakiwa inaendelea.
EmoticonEmoticon