RAIS JAKAYA KIKWETE AMEZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUWEKEZA KATIKA HUDUMA ZA KIBENKI HADI KATIKA NGAZI YA VIJIJI

 

 

Rais JAKAYA KIKWETE amezitaka Taasisi za Kifedha nchini kuwekeza katika huduma za kibenki hadi katika ngazi za Vijiji ili kusaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja na taifa kwa ujumla hali itakayochangia pia jamii kuwa na utamaduni wa kuhifadhi fedha benki.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuzindua huduma za TPB Popote inayotolewa na Benki ya Posta nchini, Rais KIKWETE amesema, ili kuharakisha maendeleo kwa jamii kupitia huduma za fedha, Serikali itahakikisha asilimia 50 ya Wananchi wanafikiwa na huduma hiyo hadi kufikia mwaka 2015.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Uchumi DK WILLIAM MGIMWA ambaye ndiye mwenye dhamana ya mabenki nchini kupitia Benki ya Tanzania BOT anazungumzia mkakati wa kuiboresha benki POSTA ili kukuza mtaji wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta nchini Profesa LETICIA RUTASHOBYA amesema ili kuendana na ushindani wa kibiashara, benki yake imepanga kuongeza idadi ya wateja kutoka laki sita waliopo sasa hadi kufikia Milioni 1.2 ifikapo mwaka 2015.
Benki hiyo imeweza kukuza kiasi cha faida yake kutoka Bilioni 3.8 mwaka 2011 hadi kufikia Bilioni 7.2 mwishoni mwa mwaka huu.

Previous
Next Post »