FAHAMU KWA UNDANI HOMA YA DENGUE ITAKUSAIDIA



Ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na  kuambatana na maumivu makali, husambazwa na mbu aina ya Aedes na husababishwa na virusi viitwavyo Dengue.
 Je ni wapi homa hii upatikana zaidi duniani?
•India
•China
•Visiwa vya pasifiki
•Mexico
•Afrika
 Dalili za homa ya dengue:
•Homa kali ya ghafla
•Maumivu makali ya kichwa
•Macho kuuma
•Maumivu ya viungo
•Kichefuchefu
•Kutapika
•Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza
•Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi
 Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi
 Matatizo ambayo yanaweza kutokea baada ya maambukizi ya homa hii ni:
•Homa kali zaidi
•Kuharibiwa kwa tezi na mishipa ya damu
•Kutokwa na damu zaidi puani na kwenye fizi
•Ini kuwa kubwa
•Na huweza kupelekea kifo
 Dengue
Vipimo
•Damu huchukuliwa na kuangalia virusi vya dengue au
• Kingamwili dhidi ya virusi hizi
 Matibabu:
 Mpaka sasa hamna dawa kwa ajili ya ugonjwa huu ila  dawa za kupunguza homa na maumivu huweza kutumika kwa mfano:
•Paracetamol
•Pumzika vya kutosha
•Kunywa maji
•Nenda hospitali ukapate ushauri wa daktari
 MUHIMU: epuka dawa jamii ya aspirini maana huweza kusababisha damu iendelee kutoka
Previous
Next Post »