Bunge
la Afghanistan limemfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani Mujtaba
Patang (pichani), ambaye ni mmoja wa wakuu wa usalama nchini humo, ikiwa
haujatimia ya mwaka mmoja tu baada ya kuchukua wadhifa huo.
Patang
ameondolewa kupitia hoja ya kutokuwa na imani naye iliyopigiwa kura 136
dhidi ya 60, kuhusiana na shutuma za ufisadi na kuzembea kazini katika
makabiliano na wanamgambo wa Taliban.
Waziri
Mkuu huyo ameachishwa kazi ikiwa ni mwezi mmoja baada ya serikali ya
Aghanistan kuchukua rasmi majukumu ya usalama wa nchi kutoka kwa majeshi
ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO yanayoongozwa na Marekani.
Bunge
lilimwondoa mtangulizi wa Patang, Bismillah Mohammadi mnamo Agosti
2012, kwa kudaiwa kushindwa kuitisha uasi wa wanamgambo wa Taliban
pamoja na mapigano ya mpakani kati ya nchi hiyo na Pakistan.
EmoticonEmoticon