Wacheza sinema maarufu wa Hollywood Marekani kuigiza filamu fupi ya kupiga vita silaha za nyuklia.

Michael Douglas 04

Baadhi ya waigizaji wakubwa wa sinema nchini Marekani wameunganisha nguvu zao na kutengeneza video inayotoa wito kwa dunia kutokomeza silaha za nyuklia.

Muigizaji Mkongwe Michael Douglas amesaidia katika kutafuta waigizaji kama Roberto de Niro, Morgan Freeman na Matt Damon ili washiriki katika filamu hiyo ya dakika mbili (2)

Mastaa hao ambao pia yupo Alex Baldwin, Danny DeVitto na Martin Sheers wamemtaka rais Barack Obama wa Marekani kuweka wazi mikakati ya kupunguza na kisha kutokomeza kabisa silaha hizo.

Video hiyo imetolewa  na kujikuta ikienda sambamba na mkutano wa G8 unaofanyika kaskazini mwa Ireland.

Previous
Next Post »