“PRESS RELEASE” TAREHE 21. 06. 2013.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO
TAREHE 20.06.2013 MAJIRA YA SAA 10:30HRS HUKO KIJIJI CHA KAMFICHENI- KASANGA
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MISAKO WALIMKAMATA PETER S/O MALEMA, MIAKA 28,
MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KASANGA
AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] YENYE UJAZO WA LITA 5 NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA
POMBE HIYO TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO]
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA KYELA - KUINGIA NCHINI BILA
KIBALI.
MNAMO
TAREHE 20.06.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KASUMULU WILAYA YA KYELA MKOA WA
MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA
DORIA/MISAKO WALIMKAMATA AKILI S/O
SALIM, MIAKA 25, MHUTU, RAIA NA MKAZI WA KONGO AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA
KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KUHUSU MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI..
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon