TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


 

 
“PRESS RELEASE” TAREHE 20. 06. 2013.



WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA
                                                 KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA
                                                 ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.

 

MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE .CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100, HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI. PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI. HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA . ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.

 

WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI

 

MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KIJIJI CHA MKWANGU WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA  DORIA/MISAKO  WALIMKAMATA SEMI S/O KIJA, MIAKA 40, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MKWANGU AKIWA NA BHANGI DEBE  MOJA  YENYE UZITO  WA  KGM 12 NDANI YA NYUMBA YAKE . MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

 

WILAYA YA KYELA - KUPATIKANA NA BHANGI 

 

MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO KIJIJI CHA NJISI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MISAKO WALIMKAMATA REBEKA D/O SIMBEYE, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA – SONGWE  AKIWA NA BHANGI KETE 9 SAWA NA  UZITO  WA  GRAM 45 NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

 

 

WILAYA YA MBOZI - KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.

 

MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KIJIJI CHA MPITO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MISAKO  WALIMKAMATA YAREDI S/O JIMU @ MGARA, MIAKA 45, MNYIHA,  MKULIMA, MKAZI WA MPITO AKIWA  ANAMILIKI SILAHA AINA YA GOBOLE MOJA  NDANI YA NYUMBA YAKE   BILA KIBALI.  MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

 

 

Signed By,

                                                            [DIWANI ATHUMANI   - ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 
Previous
Next Post »