Maelfu ya raia wamejiunga na maandamano nchini Brazil, kupinga gharama za maandalizi ya michuano ya kombe la dunia.
Maandamano hayo ndiyo makubwa zaidi kufanyika tangu enzi za utawala wa kidikteta nchini humo.
Polisi mjini Rio de Janeiro, imetumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira dhidi ya vijana siku ya Jumanne ili kutuliza ghasia.
Maandamano hayo yamekuja wakati wa mashindano ya kombe la shirikisho la FIFA (Confederations Cup), yaliyoandaliwa na Brazil.
Maswali yameanza kuulizwa juu ya utayari wa Brazil kuandaa matukio makubwa, iikiwemo ziara ya papa katika kipindi cha mwezi mmoja na kombe la dunia mwakani.
EmoticonEmoticon