HUYU NDIO MWANAMKE MWENYE KUCHA NDEFU ZAIDI ZA MIKONONI DUNIANI.

NewsImages/1097034.jpg


Lee Redmond, 67, mkazi wa Utah nchini Marekani alianza kuzifuga kucha zake tangia mwaka 1979 liliripoti gazeti la Salt Lake Tribune.

Alikuwa na kucha ndefu zilizokuwa na urefu wa inchi 33 zilizomuwezesha kuvunja rekodi ya dunia na kuingia katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness.

Lee Redmond alizipoteza kucha zake alizozitunza kwa takribani miaka 30 baada ya kupata ajali ya gari iliyohusisha magari manne. Kucha zake zote zilivunjika.

Lee Redmond alikuwa abiria katika gari mojawapo na alipata majeraha kadhaa yaliyomfanya akimbizwe hospitali lakini majeraha hayo inasemekana hayakuwa yakitishia maisha yake.

Mwaka 1995 Lee Redmond alidokeza kwamba televisheni moja ya Japan ilimuahidi kumpa dola 10,000 iwapo watamkata kucha zake 'live' kwenye televisheni hiyo lakini alikataa dau hilo na kuamua kuendelea kuzitunza kucha zake.

Ukitaka kuona jinsi mwanamke huyu alivyokuwa akiishi na makucha yake nenda kwenye photogallery yetu.

 
Previous
Next Post »